Shusho wakuabudiwa lyrics

 
Wakuabudiwa, wakuheshimiwa ni wewe mungu
Wakupewa sifa, na utukufu ni wewe mungu
Mungu mwenye nguvu, wastahili heshima zote
Hakuna mwingine, wakulinganishwa na wewe mungu ×2

Umesema wewe, jina lako liko na liko niwe mungu 
Unafanya mambo, yaliyo juu ya fahamu zetu mungu
Ukisema ndio, nani awezaye kupinga hakuna
Wewe unatupa, kushinda na zaidi ya kushinda
Unatupandisha,utukufu hadi utukufu mungu ×2

 

Uzima wetu, uko miikononi mwako mungu
Unawapa nguvu, wanyonge na wadhaifu mungu
Unawanyeshea mvua wema nao waovu mungu
Mwanadamu nani, wakulinganishwa na wewe mungu
Nani mwenye nguvu, wa kusimama mbele yako mungu ×2

 

Bwana utukufu wako singuse, mbali utukufu ukurudie wewe mungu wangu

Comments

Popular posts from this blog

Ahadi Zake (His Promises) by Marion Shako

Yahwe Uhimidiwe Angela chimbalonza